Wakati wa kutoa ombi la nafasi katika kipindi cha ARTISTS IN RESIDENCY (AIR) 2015 umewadia. Walio na nia ya kujishughulisha mwaka huu wanaulizwa waanze kutuma maombi yao.
Kila mwaka, Africa Centre kupitia kipindi chao cha AIR, kinawawezesha wasanii kujishughulisha kwa muda wa wiki 6-8 ili waweze kuendeleza sanaa yao. Huu mwaka tunafurahia sana kutangaza kwamba nafasi zipo ya wasanii kumi na watatu katika kipindi hiki cha AIR, tukishikana mkono na vipindi vingine katika nchi za Australia, Brazil, India, Italia, Kenya, Uispania, Tanzania na Amerika.
AIR inatoa wito kwa wasanii wa Afrika wa hali ya juu, waliojihusisha na jamii, na walio na nia ya kuvunja mipaka ya sanaa yao.
AIR itamchagua msanii mmoja kutoka orodha itakayotoka kwenye Africa Centre. Msanii huyu atajaza nafasi moja ya ukaazi ya kipindi cha 2015 au 2016. Gharama za ukaazi na kusafiri zimepangiwa katika tuzo la kipindi hiki.
Nafasi hizi ziko wazi kwa wasanii wa kila aina; iwe waandishi, wenye filamu, muziki, au waigizaji. Kila nafasi itakuwa na mpangilio wake, matakwa tofauti na muda wake.
Tuma ombi lako leo!
Tarehe ya mwisho ya kutoa ombi lako ni 31 Septemba 2015.